Sunday, May 13, 2012

KUMEKUCHA UKOMBOZI CHOIR MSASANI JIANDAE KUSIKIA KUTOKA KWAO

Ukombozi Choir wakiwa location wakirekodi huku mwimbishaji mwanadada Jenny Exaud akiwa mbele kuongoza wimbo huo.


Ukombozi choir kutoka kanisa la Kilutheri usharika wa Msasani wako busy na zoezi lao la recording ya video yao mpya,recording ambayo inafanywa na kampuni ya AJM Production inayojiongezea sifa kila kukicha kutokana na kazi yao njema katika kureekodi waimbaji binafsi,vikundi pamoja na kwaya mbalimbali ndani na nje ya nchi ikiwa chini ya mwanamama Joyce Mlabwa.

Kwaya ya Ukombozi ilizindua audio mapema mwaka huu kwasasa wanakamilisha video hiyo ambayo itakuwa na nyimbo zaidi ya nane ukiwemo Kwa neema ambao unatamba kwenye vituo mbalimbali vya radio za injili jijini Dar es salaam.Chini ya mwenyekiti wake bwana Erick Mchome kwaya hiyo tayari inatoleo la kwanza la video ambalo bado linafanya vyema kwenye soko la muziki wa injili nchini.Kwaya hii kabla ya kubadiri jina ilikuwa ikifahamika kwa jina la kwaya ya vijana msasani wakitamba na wimbo kama Nakushukuru Mungu umenitoa mbali,ambao ulitamba jijini Dar es salaam kupitia kipindi cha muziki na nyimbo za dini kinachoendeshwa na radio Tumaini.

Jiandae kupata kazi mpya ya wana Ukombozi Choir kutoka KKKT usharika wa Msasani, Dayosisi ya mashariki na pwani.


                BAADHI YA PICHA ZA KWAYA HIYO WAKIWA KATIKA RECORDING YAO.

Baadhi ya waimbaji wa Ukombozi Choir wakiwa katika picha kabla ya recording.



Hapo sasa,wana Ukombozi wakishambulia kwenye recording yao.



Kundi moja baada ya jingine,Ukombozi Choir wamejipanga haswa.


Moja ya jaribu kwa wasiojua stepu utawaonea huruma,kazi hiyo ikirekodiwa.



Wamependeza sana,recording ikiendelea.



Moja ya group chini ya mwenyekiti wa kwaya Erick Mchome kulia wakirekodi.

No comments:

Post a Comment