Tuesday, July 31, 2012

CHEMSHA BONGO NA BIBLE

Mtunzi wa Mtihani: Rulea Sanga

MITIHANI WA MWISHO WA MWEZI JULAI 2012 WA CHEMSHA BONGO NA BIBLE
Unatakiwa kujibu maswali yote kwa muda wa saa mbili na nusu. Tunaamini utazingatia hilo agizo kwasababu wewe ni mtumishi wa Mungu.

Majibu yako unaweza kunitumia katika email yangu rumatz2011@yahoo.com.

Angalia muda ulioanza kujibu kwa makini.

Kumbuka hapo ulipo unasimamiwa na Roho Mtakatifu kwahiyo huwezi kufanya jambo lakuangalizia.


Ukiangalizia Roho Mtakatifu na nguvu za Mungu zitakutoa katika chumba chako cha kufanyia mtihani.

Matokeo yako utatumiawa kwa email na utapewa na cheti cha kufanya mtihani.

Kila swali lina maksi 10

Jinsi ya kujibu: Unatakiwa kuchagua jibu sahihi na ukipata andika namba ya jibu na jibu lake kwa kuandika herufi kama ni A, B, au C. Na usiandike swali, wewe tutumie hiyo herufu na namba ya swali.


MASWALI YOTE NI YA KUCHAGUA

Chagua jibu sahihi;


  1. Kitu gani kilitokea wakati Yesu anabatizwa

                 (a) Wingu jeusi

                  (b) Tetemeko la ardhi

                  (c) Mbingu za dunia zikamfunukia akaona Roho wa Mungu akishuka             
                 kama hua, akija juu yake, na sauti kutoka juu ikisema, Huyu ni
                 mwanagu mpendwa wangu, ninayependezwa naye

  2. Yesu alipopandishwa na Roho nyikani ili ajaribiwe na ibilisi, alifunga kula siku ngapi?

                  (a) kumi

                  (b) Sita

                  (c) Arobaini
  3.   (i) Yesu alipoingia Kapernaumu, akida mmoja alimjia, akimsihi akisema, Bwana mtumishi wangu amelala, mgonjwa wa kupooza, anaumwa sana. Yesu akamwambia,

                  (a) Amini ameshapona

                  (b) Nitakuja, nimponye

                  (c) Nitakuja, nimuokoe na atapona.

    (ii) Yule akijibu akasema, Bwana mimi sistahili wewe uingie chini ya dari yangu, lakini sema neno na mtumishi wangu atapona. Yesu aliposikia hayo alistajabu akawambia wale waliomfuata

                  (a) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
                 katika Israel

                  (b) Amini na wambie sijaona imani kubwa kama hii kwa yeyote
                 katika mkutano huu

                  (c) Amini na wambie sijaona upendo kubwa kama huu kwa yeyote
                 katika Israel

  4. (i) Kuna muujiza ambao Yesu aliufanya wa kuiongeza mikate na samaki ambapo wanafunzi wake walikula mpaka wakasaza. Ni mikate mingapi na samaki ngapi ambazo Yesu aliziombea kwa kutazama juu mbinguni kwa Mungu?

                  (a) Mikate miwili na samaki watano

                  (b) Samaki wawili na mikate mitano

                  (c) Mkate mmoja na samaki waili

    (ii) Masazo yaliyobaki baada ya wanafunzi kula na kushiba ilijaa vikapu vingapi?

                  (a) kumi na viwili

                  (b) Kuma na saba

                  (d) viwili

  5. Ni baada ya kufanya nini, Yesu aliwaambia, “Imeandikwa, nyumba yangu itakuwa nyumba ya sala, bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi”.

                  (a) Ni baada ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
                 kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
                 waliokuwa wanauzia njiwa

                  (b) Ni baada ya Yesu kuingia msikitini na kuona watu wakiuza na
                 kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
                 waliokuwa wanauzia njiwa

                  (c) Ni kabla ya Yesu kuingia hekaluni na kuona watu wakiuza na
                 kununua, Yesu akapindua meza za wabadili fedha na viti vyao
                 waliokuwa wanauzia njiwa
  6. (i) Yuda alipoona ya kuwa Ysu amekwisha kuhukumiwa, alifanya nini?

                  (a) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
                 vipande thelathini na moja vya fedha

                  (b) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
                 vipande thelathini vya fedha

                  (c) Yuda alijuta akawarudishia wakuu na makuhani na wazee vile
                 vipande thelathini vya dhahabu

    (ii) Ni maneno gani Yuda alisema baada ya kurudisha vile vipande alivyopewa kwaajili ya kumsaliti Yesu?

                  (a) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu isiyo na hatia
                  (b) Alisema, Sijakosea nilipoisaliti damu isiyo na hatia
                  (c) Alisema, Nalikosa nilipoisaliti damu iliyo na hatia

    (ii) Yuda baada ya kukimbia ndani ya hekalu kutokana na kumsaliti Yesu alifanya nini?

                  (a) Alikimbia na kujinyonga

                  (b) Alirudi na kumsujudia Yesu

                  (c) Alihuzunika sana na kulia

  7. Baada ya kusikia kuwa Herode amekufa Misri, Yusufu, Yesu na Bikira Maria  walitoka Israel ni wapi walienda kuishi?

                  (a) Nazareti

                  (b) Misri

                  (c) Marekani
  8. Taja majaribu matatu ambayo Yesu alijaribiwa na Ibilisi nyikani?

                  (a) (i) Mawe yawe mikate

                      (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

                      (iii) Kumsujudia Ibilisi

                  (b) (i) Mchanga uwe mikate

                      (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha mlima

                      (iii) Kumsujudia Ibilisi

                  (c) (i) Mawe yawe mikate

                      (ii) Yesu kujitupa chini kutoka katika kinara cha hekalu

                      (iii) Kumsujudia Mfalme
  9. Yesu aliposhuka mlimani, makutano mengi walimfuata. Na tazama akaja mtu mwenye ukoma, akamsujudia akisema,

                  (a) Bwana ukitaka unaweza kunitakasa

                  (b) Bwana ukitaka waweza kunibariki

                  (c) Bwana ukitaka waweza kunihurumia

  10. (i) Taja jina la mfalme aliyemfunga na kumtia Yohana Mbatizaji gereza?

                  (a) Kayafa

                  (b) Rulea Sanga

                  (c) Mfalme Herode

    (ii) Kwani Yohana alifungwa gerezani?

                  (a)  Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye          
                 Filipo awe mke wake na Herode.

                  (b) Yohana alimwambia sio halali kwa Kayafa kuwa na nduguye
                 Musa awe mke wake na Herode.

                  (c) Majibu ya hapo juu sio sahihi

    (iii) Kwanini mfalme alipoona watu akaogopa kumuua Yohana Mbatizaji?

                  (a)  Yohana alimwambia sio halali kwa Herode kuwa na nduguye
                 Filipo awe mke wake na Herode.

                  (b) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Nabii

                  (c) Kwasababu watu walimuona Yohana Mbatizaji kama Mfalme

    (iv) Ni nani aliyecheza mbele ya Herode wakati wa sikuku yake ya kuzaliwa akampendeza Herode kwa uchezaji wake?

                  (a) Binti Herode

                  (b) Mjukuu wa Herode

                  (c) Rafiki yake na Binti Herode

    (v) Ni nani alimshauri huyu mtu aliyecheza mbele ya mfalme Herode na mpaka Herode akakubali kutimiza kiapo chake cha kumpa chochote atakachoomba?

                  (a) mama yake

                  (b) Kaka yake

                  (c) Rafiki yake

    (vi) Huyo aliyemfurahisha Herode kwa kucheza aliomba  nini apewe na huyo mfalme?

                  (a) hakuomba chochote

                  (b) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika mfuko

                  (c) aliomba kichwa cha Yohana Mbatizaji katika kombe

    (vii) Unafikiri Herode alifuarahia ilo ombi la huyu aliyecheza vizuri katika sikuku yake ya kuzaliwa? Na kama alifurahi au alisikitika ni kwanini?

                  (a) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni aibu kwa watu waliokuwa
                 nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika sikukuu yake

                  (b) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni atakimbiwa na watu
                 waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika
                 sikukuu yake

                  (c) Herode alisikitika, kwasababu aliona ni si haki na ni uonevu  kwa
                 watu waliokuwa nao katika meza ya chakula na wote waliofika katika             
                 sikukuu yake

    (viii) Baada ya kichwa cha Yohana Mbatizaji kukatwa na kukabidhiwa yule kijana alicheza vizuri mbele ya mfalme Herode, ni wapi alikipeleka hicho kichwa?

                  (a) mama yake

                  (b) Kaka yake

                  (c) Rafiki yake

Friday, July 20, 2012

ODAMA AFIWA NA MAMA YAKE MDOGO

Muigizaji wa filamu Tanzania Jennifer Kyaka (Odama) leo asubuhi amefiwa na mama yake mdogo katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam. Marehemu alikuwa amelazwa mahali pale kwa muda mrefu sana, lakini leo Mungu amempenda na  amemuchukua.



Sasa hivi zinafanyika jitihada za kuondoa mwili wa marehemu n kuelekea nyumbani kwake. Tutazidi kuwajuza ni wapi msiba utakuwepo.


Unaweza kuwasiliana na Jennifer Kyaka kwa kutembelea blogu yake ya www.odama1.blogspot.com


Wednesday, June 13, 2012

MPIGIE KURA CHRISTINA SHUSHO, IPIGIE KURA TANZANIA, IINUE AFRICA
VIVA SHUSHO....VIVA TANZANIA
Christina Shusho,akihojiana na mablogaz wa Kitanzania katika hotel ya The Atriums iliyoko Sinza Africa sana
Siku ya jana jioni mablogaz wanaomiliki blogu za Kikristo Tanzania, Rulea Sanga, Uncle Jimmy, Sam Sasali, K-Junior, Martin Macele walikuwa na mahojiano na Christina Shusho katika hotel ya The Atriums Sinza Africasana kuhusiana na shindano kubwa lililoko machochoni pa mtumishi wa Mungu Christina Shusho.

Christina Shusho alimshukuru Mungu kwa kuweza kumtumia kama chombo kufikisha ujumbe kwa jamii kwa njia ya uimbaji na pia kuweza kushiriki katika Gospel Music Awards Africa. Pia aliwashukuru mablogaz kwa kazi yao nzito wanayofanya kumtangaza katika blogs zao na kupoteza muda wao kwaajili ya kumuinua Kristo.
Aliwaomba Watanzania na Africa nzima kumchangua Christina Shusho ili kuliwakilisha Bara la Africa,Tanzania na kumuweka Kristo juu ya vyote.
Christina Shusho ni mwimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania na amekuwa chachu kwa waimbaji wenzake na kwa watanzania kwa uimbaji wake na ujumbe naoutoa ambao umekuwa na mguso katika kukarabati imani za watu.
Christina Shusho anategemea ku-perform DAR LIVE siku ya jumapili, kwahiyo amewaomba Watanzania wote kufika mahali pale na kuweza kumpigia kura, kutakuwepo na mablogaz na kompyuta zao ambapo utakutana nao na watakuelekeza jinsi ya kupiga kura....

Tukutane Jumapili Dar Live
1.Emmy Kosgei-Kenya
2.Dena Mwana – Congo
3.Ntokozo Mbambo- South Africa
4.Rebecca- UK
5.Gifty Osei- Ghana
6.Kefee -Nigeria
7.Onos Ariyo- Nigeria
8.Diana Hamilton-UK
9.Christina Shusho -Tanzania
10.Lara George- Nigeria
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA-MSIKILZE SHUSHO ALIPOKUWA ANAONGEA NA MABLOGAZ JANA THE ATRIUMS HOTEL SINZA AFRIKASANA
USIKOSE MTUMISHI WA MUNGU...NJOO TUFANYE KAZI YA BWANA KWA KUM-SUPPORT MTANZANIA MWENZETU 

KAMA ULIKUWA HUJUI KUHUSIANA NA MASHINDANO HAYA, TAFADHALI SOMA HAPO CHINI



Siku 18 zimebakia kabla ya pazia la upigaji kura kufungwa kwa waimbaji wa gospel barani Afrika, ambao wanawania tuzo mbalimbali kupitia Africa gospel music awards ambazo zinatarajiwa kutolewa siku ya jumamosi ya tarehe 7 mwezi wa 7 mwaka huu huko jijini London nchini Uingereza. Ambapo kama ilivyokuwa kwa mwaka jana mwimbaji wetu mmoja tu, ametutoa kimasomaso kwa kupendekezwa katika kuwania kupata tuzo hizo mwimbaji huyo si mwingine bali ni Christina Shusho, ambaye mwaka jana alitoka mikono mitupu lakini mwaka huu tukiungana kwa pamoja watanzania wote kwa kumpigia kura lazima atarudi na tuzo zote mbili alizopendekezwa kuwania.

Shusho yumo kwenye kuwania mwimbaji bora wa kike wa mwaka pamoja na mwimbaji bora wa mwaka Afrika ya mashariki, tuzo ambazo anawania na waimbaji wengine wanaofanya vyema kwenye gospel barani Afrika wakiwemo wakina Ntokozo Mbambo wa Afrika ya kusini na waimbaji wengine. Kikubwa ninachoweza kukwambia tukifanikiwa kuunganisha nguvu zetu kwa pamoja kwa kumpigia kura atakuwa nanafasi kubwa ya kutwaa tuzo hizo, kwasababu waimbaji wengine wanaowania tuzo hizo wengi wao wanatoka nchi moja hali ambayo itafanya kura zao kugawana kitu ambacho kitatupa nguvu ya kumwezesha Shusho kurudi na tuzo kwani Tanzania nzima kura zetu tunaelekeza kwake.

Mikakati mbalimbali inafanywa ili kuhakikisha kila mtu anashiriki katika upigaji kura kwakuwa hauhitaji kulipa ili kupiga kura, kikubwa unatakiwa ujiandikishe kwenye tovuti ya shindano hilo ambayo maelekezo yake yapo chini ya habari hii, zaidi kama nilivyoandika mikakati inafanywa ili kuhakikisha watanzania wanashiriki kikamilifu katika zoezi hili katika siku 18 zilizobaki. Hapo jana bloggers walikutana na Christina Shusho katika hoteli ya Atriums iliyopo Sinza jijini Dar es salaam ili kupanga mikakati zaidi ya kuweza kupata tuzo hizo ambazo faida yake ni kumwinua Yesu pamoja na kuitangaza nchi yetu ya Tanzania duniani. Natumai umenielewa ili kupiga kura ingia kwenye link hii na kufuata maelekezo chini yake.
http://www.africagospelawards.com/nominate.html


AGMA 2012 VOTING GUIDELINES
1. Click on the 'VOTE NOW' button.
2. Register your email address, confirm and submit.
3. Check your email (inbox) and you will find the link to vote.
4. If you do not find the link in your email inbox, please check your junk mail folder.
5. Once you have connected to the voting page please make your selections and submit (you can only vote for one nominee from each category).
6. You do not have to vote in every category.


ANGALIA BAADHI YA PICHA ZA BLOGGERS NA CHRISTINA SHUSHO HAPO JANA 
Kikao kikiendelea

Blogger Victor kulia akinukuu jambo kutoka kwa Christina Shusho
Rulea Sanga alipoamua kupiga picha ya pamoja
Shusho akieleza jambo kwa mabloggers
 Victor akizidi kuchangia nawazo yake
K-Junior akiwa busy na kuchukua maphotoz

Watumishi wa Mungu wakihakikisha kila kitu kinaenda sawa


Papaa akimuelezea Shusho mikakati ya mabloggerz kuhusiana na upigaji kura


Kutoka kulia ni Shusho, Martin Malecela pamoja na Victor Mboya wakimsikiliza Rulea Sanga akimpongeza Shusho kwa juhudi zake


Rulea Sanga akisikiliza kwa makini mchakato wa kupata tuzo ulivyo.


Mablogaz  na mchungaji aliyoko upande wa kulia


K-junior wa kwanza upande wa kulia akimsikiliza mchungaji wa Vijana


Hakika kikao kilinoga wajameni.

Unclejimmy


Kikako kikiendelea na mabloggerz Tanzania waliojikita kumtangaza Kristo

''Inuka maana shughuli hii yakuhusu wewe, uwe na moyo mkuu, ukaitende (Ezra 10;4)''.
VIVA SHUSHO, VIVA TANZANIA.

Wednesday, May 30, 2012

BABY FASHION! BABY FASHION! BABY FASHION!

DUKA JIPYA LA NGUO ZA WATOTO NA WATU WAZIMA LAFUNGULIWA MSASANI KARIBU NA  GENERAL TYRE-ULIZA BABY FASHION
Baby fashion ni duka linalouza nguo za watoto, viatu, mashati, tshirts, skni tight, vest, bangili, ereni na urembo kwa akina mama. Bei zetu ni nafuu sana, na ukifika utashangazwa na huduma utakayopata kwa kuuzwa bei poa sana. 

Hizi ni baadhi tu ya nguo tulizonzo:-

WASILIANA NASI KWA SIMU +255 712 87 33 13
BARUA PEPE: veronicajoseph90@gmail.com
Blogu: www.newbabyfashion.blogspot.com

 



















Saturday, May 26, 2012


SEND OF YA LETICIA MWAKAG'ATA KATIKA UKUMBI WA V.I.P. DIAMOND JUBILEE-DAR ES SALAAM

GLORIOUS CELEBRATION WAIPAMBA SEND OFF KWA UIMBAJI
 Bibi harusi mtarajiwa Leticia Mwakang'ata akiwaka na pink..umependeza
 Mama yake na Leticia
 Kitu khanga....zikipelekwa kwa mama yake na Leticia kwa kupongeza



 Askofu Mwakan'ata na mke wake..Hawa ni wazazi wa mhusika mkuu wa kitchen party hii Leticia
 Askofu Mwakang'ata akimpongeza mwanae kwa hatua aliyoichukua
 Leticia akimbusu mama yake kama ishara ya upendo na shukrani kwa malezi mema
 Leticia akiwa na marafiki zake
 Kushoto ni mdogoake na Leticia akifuatia mwimbaji wa Glorious Celebration

 Mama Askofu Mwakang'ata
 Wadogo zake na dada zake na Leticia, wakitokelezea

 Leticia
 Emmanuel Mabisa
 Ima Solo akiwa na solo gitaa lake
 Kutoka kulia ni Paul, Nice, Angel, Mercy na Davina
 Wapiga gitaa, Ima solo na Ima base kulia
 Mtalaamu wa kinanda, OG
 Ni furaha ndani ya Yesu
 Mercy na Davina kushoto
 Kitu suti
 Drums zilipigwa siku hiyo na mpigaji wetu
 Kundi zima la Glorious Celebration
Kitu misosi

 Mabisa na Nice hwakuwa mbali na misosi
 Mauzo..hahahahah...
 Baada ya kazi ni kuwa na marafiki..kama unavyoona watoto wa GC