Sunday, January 13, 2013

ALBAMU MPYA YA GIDEON T. MUTALEMWA IMEMALIZIKA….NA AFUNGUKA NA KUELEZA MAISHA YAKE YA UKRISTO AKIWA KATIKA KANISA LA KATOLIKI NA KUHAMIA PENTEKOSTI

Rumafrica ilitembelewa na mwimbaji maarufu sana Tanzania katika ofisi yetu iliyoko Afrikasana Sinza hapa jijini Dar es Salaam siku ya tarehe 12.01.2013. Mwimbaji huyu alieleza maisha yake ya Ukristo akiwa katika makanisa ya Kikatoliki na baadae kuhamia katika makanisa ya Kipentekosti. Pia alitueleza jinsi gani wazazi wake walivyomchulia alipoamua kuachana na dini ya wazazi wake. Mwimbaji huyu hakuishia hapo pia alitueleza kipaji chake kikubwa cha uimbaji alikipata akiwa na umri gani na vitu gani vilimfanya apende kuimba na kucheza. Matatizo aliyoyapata akiwa katoliki na matatizo anayoyapata akiwa Pentekosti

Utaweza kujua kwanini aliamua kuita albamu yake “Sambamba na Yesu”..Ni mengi utajua kuhusu mwimbaji huyu..naomba ufuatilie mahojiano haya:


 Gideon Tryphone Mutalemwa




RUMAFRICA:           Bwana Yesu asifiwe…
GIDEON:                   Amen mtumishi wa Mungu.
RUMAFRICA:           Karibu sana katika ofisi za Rumafrica.
GIDEON:                   Asante sana, nishakaribia.
RUMAFRICA:           Tungependa kujua jina lako lililoko katika cheti chako cha
kuzaliwa.
GIDEON:                   Ameni..Ninaitwa Gideon Tryphone Mutalemwa.
RUMAFRICA:           Unaweza kutuelezea kwa kifupi historia ya huduma yako.
GIDEON:                   Nilianza huduma ya uimbaji tangia nilipokuwa mdogo sana.
Nakumbuka miaka ya 1992 au 1993, ndipo nilipoanza kuimba kwaya nikiwa katika mkoa wa Kagera, parokia ya Mugala katika kanisa la Katoliki. Nilikuwa naimba nikiwa chini ya Mapadre, nikawa nafundishwa jinsi ya kuimba na jinsi ya kucheza. Nikafundishwa jinsi ya kutumia piano na taratibu za muziki, nikafundishwa kutunga nyimbo. Wakati ulivyokuwa unaendelea nikawa mzuri sana katika muziki, na baadaye nikawachaguliwa kuwa “conductor” wa kwaya na Mungu hakuishia hapo akaniwezesha kuchaguliwa na kuwa mwalimu wa kwaya.
Kwa ufupi nimeanza siku nyingi, na ninataka kusema ni kipaji kutoka kwa Mungu, kwahiyo mpaka hapa nilipofikia namshukuru sana Mungu.
RUMAFRICA:           Rumafrica ingependa kujua, wakati uko katika kanisa Katoliki na wazazi wako walikuwa wanasali hapo?
GIDEON:                   Ahaaaa..Mwana wa Mungu kama unavyojua, wazazi wanapokuzaa wanajua wakupeleke wapi pa kuabudu, kwahiyo upande walipo na wanaposali ndio mahalia ambapo unatakiwa ukulie hapo. Kwahiyo mpaka sasa naongea wazazi wangu ni Wakatoliki

 Gideon T. Mutalemwa akisisitiza jambo.



RUMAFRICA:           Kile kipaji chako cha uimbaji ulichokuwa nacho ukiwa katika kanisa la Katoliki, ni mtu alikiona kutoka kwako au kuna mtu alikushauri kuwa una kitu ndani yako na unatakiwa kukifanyia kazi?
GIDEON:                   Nikiwa Roman Catholic, niseme niligundua mwenyewe kwa kuwa nilipenda muziki. Kwanza mabali na kuwa kanisani, nikiwa mitaani nilikuwa napenda sana kusikiliza miziki ya kawaida nikiwa pia kwenye maharusi, sherehe mbalimbali, nilikuwa napenda sana kuhudhuria, nilikuwa napenda sana kucheza na kudansi. Sasa nikaona naendelea kupenda kufanya hivyo. Kwahiyo niligundua kuwa nina hicho kitu ndani yangu.
RUMAFRICA:           Ukiwa katika hali yako ya kupenda muziki kipindi hicho..Kuna watu gani ulikuwa unawapenda sana ambao ni wanamuziki na wakawa mchango katika kudumisha kipaji chako cha uimbaji?
GIDEON:                   Kwa kipindi hicho kulikkuwa hakuna kitu kama cha kupenda mwimbaji Fulani, ila ilikuwa mtu anapotunganga nyimbo, tuseme, Ndumbalo akitunga nyimbo na zikipigwa katika Parokia na kupendwa, basi zilikuwa zikisambazwa katika Parokia zote.
                                    Kipindi hicho cha nyuma, mbali ya kuwa Mkatoliki pia nilikuwa nikipenda waimbaji kama Pepe Kale, Arusi Mabellee, Sakis, Franco  na wengine wengi. Miziki Kama hiyo ikipigwa nilikuwa nacheza. Sikujua maana ya miziki hiyo, ila nilikuwa naipenda sana na najisikia rah asana.
RUMAFRICA:           Ukiwa Roman Catholic, Mapadre walikuchuliaje na huduma yako ya uimbaji na kucheza?
GIDEON:                   ahaaaa….Mapadre walinipenda, nilikuwa nao natumika pale Alutareni, ninapiga chechezo, kupiga kengere na kutoa huduma zingine alutare.
                                    Namshukuru Mungu, nilikuwa napata muda wa kuhuduma alutareni na pia kupata muda wa kufanya mazoezi ya muziki.

RUMAFRICA:           Wakati wewe ni mwalimu, wanafunzi wako walikuwa wanakuchukuliaje?
GIDEON:                   Kwakeli kipindi hicho watu walishangaa sana kwasababu nilikuwa mdogo sana. Nikawa nafundisha watu ambao ni wakubwa. Kwa kweli ilikuwa ni mshangao, ila kwa kuwa walikuwa wamenizoea katika sherehe nilizokuwa na hudhuria kwa kuwaburudisha ilikuwa kwa upande mwingine ni kawaida.
                                    Kwahiyo wenzangu walikuja kutambua mimi ni kitu Fulani ndani yangu.


 Gideon Mutalewa akijaribu kueleza aliyopitia katika maisha yake.



RUMAFRICA:           Kwa sasa hivi unapatika wapi?
GIDEON:                   Kwa sasa napatikana Dar es Salaam. Ni Mpendekosti halisi ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili na  kwa upande mwingine nafanya huduma ya APOSTOLIC.
Kwa sasa napatika katika kanisa la HUDUMA NA MAOMBEZI SALASALA, MBEZI BEACH kwa mtumishi wa Mungu Nabii Flora Peter. Hapo kanisani natumika katika upande wa Worship and Praise. Katika huduma ya uimbaji mimi ni Praise Leader na wakati mwingine wakati nakuwa sihudumu hapo kanisani, ninatoka na kuelekea mikoani kwaajili ya kumuimbia Bwana katika makongamano mbalimbali pamoja na kuhubiri.
Na zaidi nataka kuwajulisha kuwa huduma yangu hasa inalenga sana vijijini na huu ndio mzigo mkubwa nilionao. Ninapenda kufika vijiji visivyoweza kufikika.
RUMAFRICA:           Ni kitu gani kilikusababishia wewe kutoka kanisa la katoliki na kuhamia Pentekosti?
GIDEONI:                  Ninaweza kukujibu kuwa ni neema ya Mungu, unajua haya mambo. Katika suala la imani, tunapoingia katika suala la kuhofu, ni suala tunalopa kwa Mungu au ni kwa neema. Kwahiyo siwezi kusema nilipo na umri wa miaka 18 ndipo nikaamua...hapana!! Ila ni nasema Mungu anapomkuta mtu na kugumsa, basi humchomoa kutoka mahali husika anapokuwa na kumpeleka mahali Fulani kwa makusudi yake Mungu mwenyewe.
RUMAFRICA:           Wakati unamia Pentekosti kutoka kanisa la Katoliki, wazazi wako walikuwa bado wako Katoliki.
GIDEON:                   Wazai wangu walikuwa Roman Catholic na sasa bado huko huko.
RUMAFRICA:           Wazazi wako wanakuchukuliaje?
GIDEON:                   Aaaah….Mwanzoni walinichukulia vizuri, ninasema hivyo kwasababu kuna maisha nilikuwa ninaishi kama kijana, starehe za dunia kama unavyojua, usumbufu nyumbani, leo umeondoka asubuhi…umefanya kazi na labda umepita mitaa na ukanywa pombe. Kwahiyo ile pesa yako ambayo unapata kazini badala ya kuitumia kuandaa “future” yako ya baadae, unakuta inaishia kwenye maisha ya anasa zisizofaa.
Haikuwepo hofu, unafanya unachotaka kufanya. Hata kama kulikuwa na mafundisho kanisani, lakini kulikuwa hakuna ile mkazo ya kwamba “Ukifanya hivi, njia yako ni sehemu Fulani” kidogo hiyo hofu ilikuwa hamna, na hilo lazima tuwe wawazi kuwa mtu ulikuwa “free” kufanya lolote.
Tukiwa tumefanya maovu, tulikuwa tunaenda kanisani, tunafanya KITUBIO na baadae unaendelea na maisha ya kawaida.
Kwahiyo nilipookoka wazazi waliona kidogo mizigo wa matatizo umepungua nyumbani. Wazazi wangu hawakulichukulia lile swala la kuhama dini kuwa mtoto amehasi, kwani wazazi wangu walijua maisha ya walokole wanayoishi kwahiyo wakaona afadhali aende kule (Aokoke).
RUMAFRICA:           Ulipoingia sasa Pentekosti, ulianza moja kwa moja na uimbaji au kunahuduma nyingine ulikuwa unafanya na baadae ukaanza huduma yako ya uimbaji uliyotoka nayo Roman Catholic?
GIDEON:                   Mwana wa Mungu, baada ya kuwa Pentekosti, kwa kweli sikuchelewa, na kama nilichelewa nakumbuka ni wiki mbili tu…Yaani kile kitendo cha kupewa sala ya toba na kuanza kuingia kanisani na kupata yale mafundisho ya mwanzoni, moja kwa moja niliivuta ile nguvu yangu niliyokuwa nayo nafundisha na kuimba, nikajikuta na mimi natamani kusima katika kwaya kwani nilitamani kuwaona wanavyoimba na kucheza.
Niliomba nafasi ya kuijiunga na nikakubaliwa, lakini kwasababu nilizoea kuimba ile style ya Kikatoliki ya kuimba na kucheza taratibu. Kwahiyo ilichukwa muda mwingi kuendana na style za Kipentekosti, ilichukua muda kama mwezi mmoja. Na ninakumbuka nilimsumbua sana mwalimu wangu wa kwaya, maana nyimbo ikitungwa ya kwenda haraka, mimi ninaenda taratibu na ikitungwa ya haraka, mimi ninaenda taratibu.
Wanakwaya wenzangu na walimu walinipenda kwasababu nilikuwa na sauti nzuri na ninauwezo wa kuimba, ila tu miondoko ya kucheza ilikuwa inanipa shida.
Nakumbuka kwa mara ya mwisho mwalimu alipata habari zangu na kunitaka kuwa msaidizi wake nah ii ilifanyika ndani ya mwezi mmoja.


 Gideon Mutalemwa akimsikiliza mwandishi wa habari kwa makini



RUMAFRICA:           Ulipojiunga na kwaya wenzako walikuchukuliaje?
GIDEON:                   Kwa mara ya kwanza wenzangu walinishangaa sana kwasababu waliona moto umekuwa wa kasi sana. Kwasababu nilipookoka ndani ya wiki mbili nikamuomba mchungaji niingie kundini (kwenye kwaya), na mchungaji wangu alicheka sana. Mchungaji akanipeleka kanisani akanitangaza na wanakwaya wakanipokea, na siku za katikati ya wiki nikaenda kwenye mazoezi ya kuimba.
RUMAFRICA:           Ni matatizo gani ulikuwa ukiyapata ukiwa katika kwaya?
GIDEON:                   Matatizo ni mengi na changamoto ni nyingi, maneno yako mengi. Unajua unapokuwa katika kikundi kuna mamneno mengi, kudharauliana na kusema mtu huyu ni bora kuliko mtu Fulani. Mambo hayo yapo na tunayazoea na sisi ni binadamu tunatakiwa kusaidiana na kusamehana.
RUMAFRICA:           Na ni kwanini hivi vitu vya kuoneana wivu vipo, wakati tunajijua kuwa tumeokoka?
GIDEON:                   Niseme, binadamu kama binadamu kuna zile ‘behaviors’ za kibinadamu huwezi kuzikwepa hata siku moja, yaani zinahitaji neema ya Mungu kwa mtu kutambua ile “character” aliyonayo kuiondoa.
Unatakiwa utambue ile tabia na uishughulikie mwenyewe. Tunakuta na matatizo kama haya kwenye vikundi au kwa waimbakji kama sisi, kwasabau ya hali ya kutojitambua kuwa wewe ni nani. Na cha pili ni kutambua ni tabia gani iliyo ya ndani ambayo ni mbaya inayokufanya wewe usiwe na hofu na lile baya.
Watumishi wanajitahidi kuomba lakini hatuwezi kupata majibu mazuri kama yule mtu unayemuombea hajajua tatizo lake. Ninachotakka kusema ni mtu kuchukia yeye mwenyewe ile tabia aliyokuwa nayo.
Kwahiyo hatuwezi kuwakosa watu kama hao kama hawajajiachilia wenyewe Mungu kushughulikia.
RUMAFRICA:           Ni faida gani umezipata ukiwa katika kwaya ya Kipentekosti?
GIDEON:                   Faida nilizopata ni kujifunza mengi,
1.      Kama nilivyosema kuwa kuna tabia zilizotofautiana. Nikiwa Romani nilikuwa na tabia za kule na nilipoingia Pentekosti nimepata tabia za Kipentekosti. Nilipoingia Pentekosti, nilidhani ukishaokoka hakuna yale maneno ya kusemana vibaya, lakini nilipoingia nikayakuta niliyoaacha Romani. Nikaja nikagundua kuwa kama mwanadamu ili ujiweke huru ni wewe kujitambua na kusoma Neno la Mungu ili likuweke huru na haya maovu yote.

2.      Faida nyingine ni ile kuzoea, ile style ya uimbaji na kucheza  niliyokuwa natumia Romani Catholic ikabidi ibadilike.

3.      Baada ya kuzoea ile style mpya ya uimbaji na kucheza (ya Kipentekosti), nikaona sasa naweza kusimama mimi kama mimi na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji na kucheza kama “SOLO ARTIST”.
RUMAFRICA:                       Wakati sasa unahama kutoka katika kwaya na kuanza kusimama kama Solo Artist (mwimbaji wa kujitegemea), ulikuwa na uishi Bukoba au Dar es Salaam?
GIDEON:                               Mhhh!!…anyway..niseme sikuwa nahama kwaya na kuanza kuwa solo artist. Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa nafundisha nyimbo za Kiswahili nchi ya Uganda katika kituo kimoja kinaitwa Kaukuu Entebe Road katika huduma inaitwa Mount Save Ministry, nakumbuaka mchungaji wangu alikuwa anaitwa Deo, kwahiyo nilikuwa nikiimba halafu nikimaliza kuimba natoka naenda studio, na kuna nyimbo nyingi niliziimba na sikuweza kuzitoa studio, kwasababu nilikuwa naimba ili kujua ninauwezo gani wa kuimba. Ila nilitoa nyimbo kama mbili na kuziachia radioni huko Karagwe na zikawa zinapigwa sana.Baada ya kutoka Uganda, ndipo nilipokuja Dare s Salaam, nikaa kama miaka miwili na baadae niakaanza kujipanga na kuona ninawezaje kuingia studio.

 Gideon T. Mutalemwa akitafakari ya kumjibu mwandishi wa habari



RUMAFRICA:                       Vipi maisha yako ya muziki ukiwa “Solo Artst?”

GIDEON:                               aaah..kwa kweli kwa sasa nina albamu yangu ambayo ni
                                                Audio na Video. Albamu yangu inaitwa SAMBAMBA
                                                NA YESU.
RUMAFRICA:                       Kwanini ulimamua jina la albamu yako kuitwa jina hilo?
GIDEON:                               Nakumbuka Ilikuwa siku moja, tulikuwa kanisani kwetu, kuna mtumishi mmoja alikuwa akihudumu pale kanisani kwetu na badae alifariki. Alipofariki mchungaji akatuambie twende kwenye mkesha kwaajili ya kuwatia moyo wafiwa, na usiku kikundi changu cha Praise kikawa kinaendesha sifa mida ile ya usiku.
Sasa wakati naongoza sifa nikawa ninaimba mapambio. Yakaja maneno na “melody”  Nikajisikia kuguswa kutoka katika nafsi yangu. Hata kama nilikuwa sijui yule mtumishi aliyekufa uhusiano wake na Mungu, ila mimi kama mimi nilijua kuwa yule mtumishi ameondoka na ameenda kwa Mungu moja kwa moja.
Ikanijia sauti palepale ninapoimba, mguso wa Mungu niliupata nikaona ya kuwa hakika yume mtumishi ameenda mbele za Mungu pamoja na Kristo, ndipo likanijia neno “Sambamba na Yesu” pamoja na “Melody”
Kwahiyo ilipokuja ile melody na ukiangalia nilikuwa na “beat” nilizokuwa nimeziweka kati “flash”, nikaweza kuimba ile nyimbo muda huo huo usiku LIVE. Na mpaka leo waimbaji wenzangu wa Praise Team hawakumbukagi kuwa hii nyimbo ilipatika wapi, mahali gani na muda gani!!! Nakumbuka ile nyimbo nilipata usiku kama saa saba au saa nanei usiku.
Nilikuwa naimba ile nyimbo kwa machozi mazito sana. Kwahiyo nikawa najua huyu mtumishi ameondoka na Kristo..
Kwahiyo nikarudisha nyuma na kusema hata kama sio kufa, bado kuna yale maisha tunatakiwa kuishi kama wana wa Mungu. Au kama wanadamu kwa ujumla, tunatakiwa kuishi maisha pamoja na Kristo. Kila kitu tunachotaka kufanya tufanye pamoja na Kristo, tunapoongea, tunapokula.
Ninakaona niimbe hii nyimbo na itaenda kugusa mioyo ya watu. Hata kama kuna majaribu mengi tunakutana nayo.

 Gideon T. Mutalemwa akiwa na furaha na amani wakati wa mahojiano na Rumafrica



RUMAFRICA:                       Albamu yako ina nyimbo ngapi?
GIDEON:                               Ina nyimbo nane:
1.      Haleluaya
2.      Usalama uko kwa Yesu
3.      Utukuzwe
4.      Roho wa Bwana
5.      We Praise
6.      Nataka niseme na wewe
7.      Ni wewe peke yako
8.      Ntaya Yesu wange (Yesu wangu)- Hii ni nyimbo ya lugha ya Kihaya ambayo ni Lugha yangu

RUMAFRICA:                       Katika albamu yako ni nyimbo gani unaipenda?
GIDEON:                               Ha…!! Ninazipenda nyimbo nyingi, na ninashindwa nichangue ni nyimbo gani…!!! Lakini naipenda sana “Sambamba na Yesu” kwasababu nakumbuka nnipoimba studio wakati wa kurekodi, nilitokwa na machozi, nilijikuta naimba mpaka “Producer” simuoni, na Producer alishakata kompyuta kwani muda umeisha, mimi ndo kwanza naendelea kuimba na machozi yananitoka.


Gideon Mutalemwa ni mtumishi wa Mungu aliyejitoa kwa kazi ya Mungu



RUMAFRICA:                       Ni studio gani umefanya kazi yako ya audio na video?
GIDEON:                               Audio nimefanya katika mazingira magumu sana, na nimefanya katika studio nyingi kwahiyo ninashindwa kusema nimefanyia studio fulani. Ila amenifanyia mtu wa Mungu anaitwa Producer Itika, alikuwa akifanyia katika studio mbalimbali. Na mara nyingi alikuwa akinipigia simu kuwa uko wapi, naomba leo uje tukafanyie studio Fulani.
Video nimefanyia katika studio inaitwa MEDIA 55, bwana mmoja anaitwa Delick au Mr. King.
RUMAFRICA:                       Ni matatizo gani uliyapata wakati wa uandaaji wa albamu yako hii ambayo kwa sasa imekamilika?
GIDEON:                               Kwanza ni mtaji wa kuingia studio, nauli ya kwenda studio na kurudi.

Pili, upande wa video ni jinsi gani ya kuwalipa na kuwaandalia chakula. Kuwasumbua wapiga picha kutoka Location moja na kwenda location nyingine.

Tatu, kukosa watu wa ku-sponsor huduma yangu. Ila ninamshukuru Mungu kwa kuwainua watu walioweza kunisaidia
Nne, kuna tatizo ambalo limekuwa likiniumiza sana nafsi yangu, ni kwamba kuna watu wengi walikuw wameniahidi kuwa kazi yangu ni nzuri na watasimama na mimi, mtu anakuahidi kuwa njoo sehemu Fulani au muda Fulani nitakutumia pesa, unapompigia simu mara hapokei. Yaani unamwamini anapokutia moyo.

Nikaja kutambua kuna wapendwa waongo, walikuwa wanasema watakusaidia na hwakusaidii. Na mimi nilikuwa nawategemea kuwa na wana wa Mungu ambao nilikuwa nawaamini lakini sio waaminifu mbele yangu na mbele za Mungu.
Lakini nimekuja kujua nimezidiwa na watu ambao sikutegemea, yaani mtu yupo tu..mpo naye kanisani lakini apoona unaomba kitu, anaguswa na kukusaidia.
Kwahiyo nimetokea sana kutomtegemea sana kumtegemea mwanadamu kwa kiukweli wanaangusha. Lakini Mungu anaweza kumtumia mtun yeyote usiyemtarajia, kwahiyo Mungu ndiye anayenisaidia.
Nilikuwa naumia kwanini watu wa Mungu wananidanganya, lakini nikawa nasaidia na watu mbali ambao hawana Mungu.

RUMAFRICA:                       Kutokana na hayo matatizo yako, nin unawambia watu wote duniani?
GIDEON:                               Mimi ninamshukuru sana Mungu kwani najua kuwa jaribu halimpati mtu kama sio kiwango chake. Kwahiyo majribu yangu kama ya kudanganywa na watumishi. Mtumishi anaponidanya mimi siwezim kuumia sana, kwasababu sisi watumishi tunatumika kwa huyo tunayemtumikia, kwahiyo kama tunayemtumikia yupo ambaye ni MUNGU wa vyote, ambaye ndiye anayemtumia yiule asiyemwamini kwa kusaidia kazi yake, na wewe unayemjua Mungu unashindwa, ni jambo la kujiuliza sana.
Ninachotaka kuuambia ulimwengu ni kwamba ile hali kidogo haikunipa shida, nilijua kwamba anaponipitisha hapa ili mimi niendelee kujifunza kuwa yeye anatengeneza njia.
Kwahiy wale wote walioniahidi kuwa wanisaidie na wakashindwa wasidhani nimekwazika, labda ulikuwa sio mpango wa Mungu wao kunisaidia.
RUMAFRICA:                       Umeoa?
GIDEON:                               Nimeoa mke mmoja na nina mtoto mmoja na mke wangu anaitwa Maryy na mama wa maombi, na ndiye anayenifanya niwe hivi
RUMAFRICA:                       Ni kitu umepanga kwa mwaka huu katika huduma yako ya uimbaji?
GIDEON:                               Kwanza albamu yangu itakuwa karibu na ni ndani ya  miezi miwili itakuwa sokoni.
Ninaomba watu wajiandae kuja kuipokea na kitu cha pili nimejipanga kufanya uzinduzi ambao nitaanzia hapa Dar es Salaam, katika kanisa la Yesu Kristo la Huduma ya Maombezi kwa Nabii Flora Peter. Na itakuwa tarehe 3.3.2013 kuanzia saa 8 mchana mpaka saa 12 jioni baada ya ibada na hakutakuwa na kiingilio chochote.
Kama unavyosikia misemo yetu wanasema, Mtenda Kwako Hutunzwa, ninawaomba, ndugu zangu wana kagera wote, tutiane moyo katika huduma hii ya Mungu ambayo ninayo ndani yangu. Ninaomba ujue tumsifu Mungu kwa lugha ya kikwetu.
Watanzania wote kwa ujumla ninawaomba sana, mimi ni kijana wenu, mje hiyo siku ili tuweze kumtukuza Mungu na kumuabudu kwa pamoja.


Gideon Mutalemwa ni Baba mwenye mke mmoja na mtoto mmoja.



RUMAFRICA:                       Unawashauri nini waimbaji kama wewe?
GIDEON:                               Ninachotaka kuwaambia waimbaji na watu wengine, ni kuhusiana na lugha inayotumika mitaani kwetu sisi waimbakji inayoitwa WASANII.
Tumekuwa tukiitwa jina hilo na waimbaji wengi walikuwa wakilikataa pasipokujua ya kwamba haiwapasi walikatae.
Wanaitwa WASANII ni kwasababu, msanii ni mtu yeyote anayeweza ku-create kitu chochote kama mtunzi, mchoraji na wengine wengi katika ulimwengu na anaitwa yule ni MSANII.
Lakini wanatuita wasanii kwa maana nyingine, kwani wengi wanasema wasanii wanataka sana pesa. Hebu haya yote tuyaweke pembeni, ninachotaka kusema kama Gideon, ninaomba tujitambue kuwa sisi ni watumishi wa Mungu. Kwa maaana katika Biblia tunaposoma kuanzia Agano la Kale, tunakutana na habari ya kwamba, “Walipokuwa Makuhani ndipo walipokuwa Walawi.” Walawi walikuwepo kwaajili ya kuwabeba Makuhani. Kwahiyo tunapokuwa Walawi wasiopenda kupenda na kushirikiana, kwa kweli kazi ya Mungu hatutaifanya.
Ili tulikatae hilo jina la Wasanii, na tuitwe Watumishi wa Mungu, tunatakiwa kuwa na ushirikiano, umoja na kupendana.
Kuna usemi mmoja unasema “Ma-underground”, hilo jina mara nyingi linasababisha kuwa na maumivu makubwa ndani ya moyo wangu.
Kwa habari ya kutumika mbele za Mungu na Mungu anapomchagua mtu, haangalii udogo wa mtu. Ninaposema hivyo, nina maanisha anaweza kuwa mdogo kiumri au ni mdogo katika huduma yake na Mungu bado hajaanza kumuinua.
Kwahiyo wale walioko juu wasione sisi tulioko huku chini hatuweze kufanya chochote. Tunauwezo kufanya chochote na kuweza kuwasaidia hawa walioko juu.
Ninachokiomba…hebu mtupende. Maana kuna watu wengi wanalalamika sana hapa mjini na tuachane na mikoani, wanasema, “Sisi ma-underground tumekuwa tukitengewa, hatuhusishwi kwenye matamasha, na utakuta wale wakubwa wamejitenga na wako peke yao.” Yaaani hata mbele za Mungu sio haki na ninaimani Mungu hapendi.
Kwahiyo naomba tupendane, tushirikiane. Haata kama ni wadogo wanaweza kumwasaidia watu.
Nakumbuaka daudi anaenda kupigana na Goliati, baba yake alimwambia avae nguo za kiaskari aonekane askari ili akapigane. Lakini Daudi hakuweza kuvaa yale mavazi, na akamwambia baba yake naomba niende na mavazi yangu; akayavua yale magwanda akayaweka chini. Nimetoa huu mfano nikiwa na maana hii, kwamba mimi naweza nikaonekana mdogo, kwa uwezo wangu siweze kufanya chochote na ukashangaa nafanya makubwa.
Ninachowaomba ni kwamba, mtupe nafasi, na tunauwezo wa kushirikiana, tukakaa pamoja, tukajenga tukawa pamoja.
  
Halafu kingine kuna chama cha CHAMUITA, tumejiunga pale. Wapo waimbaji wakubwa na wapo waimbaji ambao ni wadogo. Kwa ufahamu wangu ni kwamba na sisi ma-undaground tunatakiwa kuonekana kuwa tunafaa katika uimbakji wa nyimbo za kumtumikia Mungu, ili tuwe karibu na dada na kaka zetu ili tushirikiane kujenga mwili wa KRISTO.

Nembo ya CHAMUITA


Stella Joel akimwimbia Mungu katika kanisa la Nabii Flora
Albamu ya stella Joel upande wa nyuma



Ninachotaka kusema ni kwamba kuna vitu vingi tunaweza kusaidiana. Gideoni leo ni underground lakini dada yangu, Stella Joel amenishirikisha katika albamu yake ya “Hakuna mwanamke Mmbaya”  katika albamu hiyo nimeimba nyimbo ya pili inaitwa “Nakushukuru Mungu”
Mimi ni mdogo kimuziki, lakini dada yangu aliona ninakitu cha thamani ambacho kinaweza kumfaidisha na tukashirikiana katika kuujenga mwili wa Kristo. Ile nyimbo sijifagilii lakini nimeimba vizuri sana. Kwahiyo namshukuru Mungu kwani katika waimbaji wote walioimba mle ni mastaa na mimi ndiye “underground” pekee.
 


Katika albamu hiyo kuna.
1.      Rose Muhando
2.      Addo Novemba
3.      Stara Thomas
4.      Faraja Mutaboba
5.      Upendo Kilahiro
6.      Victor Mwana wa Aron
7.      Deogras Pius (DP)
8.      Lakini Gideon Mutalemwa yumo.
 Tunaweza kuwa wadogo lakini tukawa na vitu kutoka kwa Mungu ambavyo vinaweza kukusaidia na wewe mkubwa katika kuujenga mwili wa Kristo.



MAHOJIANO YANAENDELEA
Unweza kuwasilia na mwimbaji huyu kwa
KANISA LA YESU KRISTO LA HUDUMA YA MAOMBEZI MBEZI SALASALA-DAR ES SALAAM, EAST AFRICA.
KWA NABII FLORA PETER
 Simu +255 719 697252 au +255 684 615423
Barua pepe: sambasambanayesu@gmail.com
Blogu: www.nabiiflora.blogspot.com
            www.rumaafrica.blogspot.com