Thursday, May 10, 2012


JIPATIE TSHIRTS, CAPS, NA WHEEL COVER SIKU YA UZINDUZI WA ALBAMU MPYA "SHETANI IMEKULA KWAKO"-ISAYA MSANGI
Akiongea na blogger wenu,Rulea Sanga, mtumishi wa Mungu Isaya Msangi amesema anategemea kuzindua album yake inayoitwa "Shetani imekula kwako" kwa lengo la kuchangia wagonjwa wanaosumbuliwa na ugonjwa wa cancer katika hospitali ya Ocean Road Dar es  

Mbali na uzinduzi pia ameamua kutengeneza Tshirts, kofia na wheel cover ambazo zitauzwa mahali hapo ili kupata fedha ya kutosha ili iweze kuokoa maisha ya ndugu zetu. Amewaomba watanzania kujitokeza na kushirikiana katika kum-support. 

Isaya Msangi alimshukuru sana designer wa kazi zote, Rulea Sanga kwa kazi nzuri aliyoifanya kuhakikisha kazi ya Bwana inasonga mbele. Kama ungependa kuwasiliana na designer huyu wasiliana naye kwa simu: + 255 715 851523 au barual pepe: rumatz2011@yahoo.com pia unaweza tembelea blog yake www.rumaafrica.blogspot.com

Kama ungependa tshirts, kofia, na wheel cover wasiliana na Isaya Msangi kwa simu: +255 719 385779 au barua pepe: isayamsangi@yahoo.com pia blogu: www.isayamsangi.blogspot.com



Kasha mbele
 Kasha nyuma
--------------------------------
Dr. Isaya Msangi amekuja kummaliza shetani kwa kumtwanga kwa wimbo wenye ujumbe mkali ambao unamsumbua shetani kila ukipigwa maredioni na  shetani amebaki akishangaaa na kukosa nguvu za kuwavamia watoto wa Mungu. "Shetani imekula kwako" ndiyo albamu ya Dr Isaya Msangi ambayo itazinduliwa na sasa iko sokoni.

Tamasha litafanyika:        Biafra-Kinondoni jijini Dar es Salaam
Muda:                               Saa 1:30 mchana mpaka 12:30 jioni
Tarehe:                              03-06-2012
Kiingilio:                          Hakuna kiingilio

Waimbajiwatakaoshiriki:  Faraja Ntaboba, Charles Thobia, Malya, Daniel Thomas, Math Baraka, Jennifer Mgendi, Sifa John, Bony Mwaitege, Sarah Mvungi, DP,  Victor Aron, Enock Jonas, Sam Kabata, Unit Family, Overcomers Singers na wengine wengi






No comments:

Post a Comment